Idadi ya watoto ambao wamepata chanjo ya Polio katika kaunti ya Kisii kufikia sasa iko katika kiwango cha chini zaidi ikilinganishwa na matarajio ya idadi iliyotarajiwa.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akizungumza nasi siku ya Jumatatu katika hospitali ya Mafunzo na Rufaa Kisii, mkurugenzi wa afya katika kaunti ya Kisii Geoffrey Ontomu alisema kufikia sasa idadi ya watoto ambao wamepata chanjo ya polio iko chini zaidi.

Ontomu alisema walikuwa na lengo la kuwachanja watoto zaidi ya laki mbili unusu lakini kufikia sasa ni chini ya 80,000 tu ndio wamechanjwa tangu zoezi hilo lilipo anza rasmi mnamo siku ya Jumamosi huku wakitarajiwa kufungasha shughli hiyo hapo kesho.

“Tunastahili kusaidia watoto walio chini ya miaka mitano ili wote wapate chanjo lakini idadi ambayo imejitokeza ni chache zaidi na kuwa ngumu kufikia lengo letu,” alisema Geoffrey Ontomu.

Ontomu pia aliomba wazazi kujitokeza kuwaleta watoto wao ili kuzuia ulemavu ambao husababishwa na ukosefu wa chanjo ya Polio.