Shule zote za serikali nchini zimeombwa kutowalazimisha wanafunzi kuabudu katika siku fulani, huku zikifahamishwa kuwa kila mtu yuko na uhuru na haki ya kuabudu siku anayoitaka.
Hii ni baada ya kubainika kuwa baadhi ya shule ambazo ni za kikatoliki hulazimisha wanafunzi wote kuabudu siku ya Jumapili, huku zile za kiadventista zikilazimisha wanafunzi wote kuabundu siku ya Jumamosi.
Akizungumza siku ya Ijumaa katika mahojiano kupitia redio ya Egesa Fm, waziri wa elimu Fred Matang’i alomba shule kutowalazimisha wanafunzi kuabudu, na kusema wale wa kuabudu Jumamosi na Jumapili wapewe fursa na uhuru wa kuabudu siku hizo.
“Hakuna haja kwa walimu kulazimisha mwanafunzi kuabudu siku ile shule hiyo inaabudu, kila mwanafunzi apewe fursa ya kuabudu siku yake iwe ni Jumamosi au Jumapili,” alisema Matiang’i.
Aidha, Matiang’i alipongeza makanisa kwa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha elimu imesonga mbele katika taifa la Kenya
“Makanisa yamekuwa yakipigania mashule kuinua elimu na ni kazi nzuri wanafanya na waendelee hivyo hivyo ,” aliongeza Matiang’i.