Wakaaji wa Pondamali katika eneo bunge la Nakuru Magharibi wanakila sababu ya kutabasamu baada ya kupokea shillingi millioni sita kutoka kwa mfanyabiashara ili kukubaliana na madhara ya mvua kali iliyoleta mafuriko katika eneo hilo.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wakizungumza Ijumaa baada ya mhisani huyo kuzuru eneo hilo, wananchi walisema wanafuraha kwa mfanyabiashara huyo kwa kuwajali kwa kuwatengea kitita hicho ili kuleta maendeleo katika eneo hilo.

Shdrack Otieno ambae ni mfanyabiashara wa duka la kuuza makaa, alitaja David Karuri kama mfanyabiashara ambae anayejali wananchi wa chini kwa kuwatatulia shida zinazoletwa na mafuriko katika eneo hilo pindi kuna mvua.

Kulingana naye, wamepokea shilingi millioni sita tayari shughuli za kurekebisha mitaro ya uzoa tayari ishang'oa nanga.

“Tumepokea fedha hizo na tumeanza kurekebisha madibwi yanayobeba maji pindi kunyeshapo. Tumepata ajira na pia swala za mafuriko imepungua kwa muda,” alidokeza Mary Kamau, alisema ni vyema kwa wananchi kupokea miradi kama hizo kwa kutatuliwa shida zinazowakumba.

 “Tumepata suluhu kwa swala la mafuriko katika eneo hili la Pondamali. Tunalilia wahisani wengine kujitokeza na kusaidia.”

Akizungumza katika eneo la Pondamali baada ya kuzuru miradi mbali mbali mhisani huyo alisema ipo haja jamii kufanyakazi kwa pamoja ili kuleta njia mbadala ya kutatua shida zinazokumba wananchi.