Askofu wa jimbo katoliki la Nakuru Maurice Muhatia Makumba amewataka wakenya kuwa waangalifu wanapowachagua viongozi kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Akizungumza kwenye hafla ya kuchangisha fedha za kufanikisha mradi wa akina mama wa muungano wa akina mama wa kanisa katoliki wa CWA ( Catholic Women Association) wa ujenzi wa makaazi ya muda ya wasichana ( hostel) katika ukumbi wa shule ya upili ya Nakuru day Jumamosi wiki jana, askofu Muhatia aidha amewahimiza wakenya kuwapigia kura viongozi wazalendo na wanaomcha Mungu.
Wakati huo huo,, alitaka wanaotaka kuchaguliwa kwenye viti vya kisiasa kutonyimwa nafasi hiyo huku akikariri kuwa wakenya wanafaa kuwasikiza lakini kufanya uamuzi wao wenyewe wakati wa kupiga kura.
"Tuwape watu nafasi ya kuwania viti vya uongozi na kuomba kura. Nawasihi mnpigie kura viongozi waadilifu na watu ambao wanapenda nchi na kuheshimu Mungu," alisema askofu Muhatia.