Daktari Evans Nyatigo anyetarajia kuwania ugavana katika kaunti ya Nyamira ameitaka serikali yakitaifa kuongeza kiwango cha pesa za maendeleo zinazopokezwa maeneo ya uwakilishi bunge kote nchini ili kuwezesha maeneo hayo kuwafadhili watoto werevu wanaotoka katika familia maskini kupata elimu.
Akihutubia wakazi katika chumba cha mikutano huko Ramba siku ya alhamisi, Nyatigo alisema kuwa shule nyingi za umma hasua vyuo vya kiufundi na maabara kwenye shule za upili zimejengwa kupitia kwa pesa hizo za CDF, hali aliyosema inastahili kiwango cha pesa hizo kuongezwa hata zaidi ili kufadhili miradi mbalimbali mashinani.
"Pesa za maendeleo bunge ni muhimu sana katika kustawisha maendeleo mashinani na ninaamini kuwa iwapo serikali yakitaifa itaongeza kiwango cha pesa hizo zinazotumwa mashinani basi tutakuwa mbali zaidi kimaendeleo kama kaunti," alisema Nyatigo.
Nyatigo aidha alisema kuwa mgao wa pesa hizo umesaidia pakubwa kuwafadhili watoto maskini wanaosomea katika shule za bweni akiongezea kuwapa changamoto viongozi wakisiasa waliochaguliwa kwenye uchaguzi mkuu uliopita kufanya maendeleo waliyoahidi wananchi wakati wa kampeni au wasichaguliwe tena kwakuto tekeleza ahadi zao.
" kwa kweli pesa za ustawishaji maendeleo bunge zimewasaidia pakubwa wanafunzi wanaotoka katika familia zisizo na uwezo wakiuchumi kupata elimu kwenye shule za bweni na ninawapa changamoto viongozi wa kisiasa kutekeleza miradi ya maendeleo ndio iwawie rahisi kuchaguliwa tena kwenye uchaguzi mkuu ujao," aliongezea.