Alikiba, msanii mashuhuri kutoka Tanzania alijumuika na Waislamu wenzake mjini Mombasa kusherehekea sikukuu ya Eid-ul-Adha, katika msikiti wa Masjid Ummu Kalthum.

Share news tips with us here at Hivisasa

Alikiba alikuwa mmoja wa wasanii tajika waliotumbuiza umati kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka kumi tangu kubuniwa kwa chama cha ODM mjini Mombasa katika uwanja wa Mama Ngina.

Msaani huyo alikuwa ameandamana na wanasiasa wakuu wa eneo la Pwani ikiwemo Gavana wa Mombasa Hassan Joho na Seneta wa Lamu Abu Chiaba.

Hii ni mara ya pili ndani ya muda usiozidi miezi miwili kwa Alikiba kuzuru mji wa Mombasa.