Mwakilishi wa wadi ya Magenche kaunti ya Kisii Timothy Ogugu amewashauri wanakandarasi wa kukarabati barabara za wadi hiyo kukarabati barabara hizo kwa njia ya halali ili pesa za mwananchi zipate kutumika vizuri.
Hii ni baada ya barabara ya kutoka eneo la Riokindo-Kiabugesi katika wadi hiyo ya magenche kutokarabatiwa vizuri na kuagizwa kwa wanakandarasi wa barabara kuikarabati vizuri kwani kuna sehemu ambazo ukarabati huo hukufanywa vizuri.
Akizungumza siku ya Jumapili alipotembelea ukarabati wa barabara hiyo, Ogugu aliomba wanakandarasi hao kufanya kazi waliyokabidhiwa vizuri ili pesa za mwananchi zitumike vyema.
“Ukarabati wa barabara unafanywa kupitia pesa za mwananchi na ni haki kwa wanakandarasi kufanya ukarabati huo kwa njia ya halali,” alisema Ogugu.
Aidha Ogugu aliomba wakaazi kushirikiana pamoja kufanya maendeleo mengi katika kaunti hiyo, huku akisema umoja ni nguvu ambayo itasongesha kaunti hiyo mbele kimaendeleo.
“Naomba kila mkaazi kushirikiana na viongozi wote wa kaunti hii ili tufanye maendeleo mengi ambayo ni ya kutunufaisha sisi wenyewe,” aliongeza Ogugu.