Takriban watu 40 wametiwa mbaroni katika eneo la Mshomoroni, eneo bunge la Kisauni, katika opareshepni dhidi ya pombe haramu na matumizi ya dawa za kulevya.
Akithibitisha kisa hicho siku ya Jumanne, Naibu mkuu wa polisi katika eneo la Kisauni Walter Abondo, alisema kuwa watu hao watafikishwa mahakamani siku ya Alhamisi ili kujibu mashtaka hayo.
Abondo alisema kuwa wataendelea na operesheni hiyo hadi pale watakapohakikisha kuwa biashara hiyo ya pombe haramu imekomeshwa kabisa katika eneo hilo.
Machifu kadhaa na manaibu wao wameachishwa kazi kwa kushindwa kusitisha biashara hiyo haramu katika maeneo yao, baada ya Rais Uhuru Kenyatta kutangaza vita vikali dhidi ya pombe haramu humu nchini.