Zaidi ya asilimia 60 ya vijana kutoka kwa familia za kurandaranda mitaani katika Kaunti ya Mombasa huenda wamejiunga na makundi ya itikadi kali ama makundi ya kigaidi kama vile al-Shaabab.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Haya ni kwa mujibu wa ripoti ya utafiti uliofanywa na shirika la kijamii la Huria, ambalo hujihusisha sana na masuala ya vijana .

Akizunguza ofisini mwao mjini Mombasa siku ya Ijumaa, wakati wa kutolewa kwa ripoti hiyo, Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo, Yusuf Lule, alisema kuwa huenda asilimia hiyo iwe juu zaidi mwakani iwapo serikali haitatafuta mbinu ya kuwazuia vijana hao kujiunga na makundi hayo.

“Kuna uwezekano kuwa vijana hao hupewa ahadi ya pesa na maisha mazuri kuliko yale ya mitaani iwapo watajiunga na makundi hayo,” alisema Lule.