Watu wanane walijeruhiwa vibaya katika kivuko cha feri siku ya Alhamisi huku magari kumi yakiharibika vibaya baada ya lori moja kugonga magari yaliyokuwa katika foleni ya kuingia ndani ya feri.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Walioshuhudia kisa hicho wanasema breki za lori hilo ambalo lilikuwa limebeba vifaa vya ujenzi zilifeli jambo lililomfanya dereva huyo kushindwa kulidhibiti kwani lilikuwa limebeba kupita kiasi.

Hata hivyo wanaotumia kivuko hicho wanaitaka mamlaka ya Kenya Ferry kuhakikisha kuwa wanakagua vizuri uzani wa mizigo ambayo magari yanabeba ili kuzui visa kama hivyo kushuhudiwa.

“Hii sio mara ya kwanza kwanini gari zibebe mizigo kupita kiasi wakati hapa feri kuna sehemu maalum ya kupimia uzani, kuna mwaka mwingine hapa trela liliuwa karibu watu kumi na hakuna hatua iliyochukuliwa,” alisema Rajab Juma mmoja wa wakaazi.

Majeruhi wa mkasa huo walipelekwa katika hospitali ya Coast General kwa matibabu huku magari yaliyoharibiwa yakipelekwa katika kituo cha polisi cha likoni.