Jiji la Mombasa lina mitaa mingi yenye sifa za kustaajabisha.
Mtopanga na Bombolulu ni baadhi ya makazi ya kaunti 001 yenye vioja. Sifa za sehemu hizi zimebanwa na wanaoishi hapa kwa minajili ya kuhifadhi jina zuri ambalo halipo.
Bombolulu ni kituo cha mnazi Mombasa. Ikiwa unahitaji kupata mnazi kama unaonywewa vijijini, tembea mtaa huu.
Tofauti ya kijijini na hapa ni ukosefu wa heshima kwa mila na desturi za kipwani mingi isipokuwa kushabikia mnazi. Vile vile, hapa utapata wanaofanya kazi ya ulinzi wengi sana hadi watu husema hapa ndipo mahali penye usalama wa hali ya juu zaidi Mombasani.
Ukitembea Mtopanga utakutana na ukweli wa mambo jinsi familia zinaendelea kudidimia. Vijana wa hapa wameishi na wazazi wao hadi wameanza kezeekea kwao.
Wanaogopa majukumu ya kulipa kodi na kujitegemea. Wengine wamezalisha na kuzalia kwa vyumba vidogo vidogo vya wazazi wao. Semi ‘Utahama lini?’ ni msamiati wa kawaida sehemu hii ya jiji.
Kwa upande wake, Sabasaba pia ni mtaa tajika Mombasa. Kwa wale wenye tamaa ya ‘nyama mtu’ kwa bei nafuu, tembea huku. Madanguro yasiyobagua tajiri au maskini yapo hapa.
Hii imekuwa sababu kuu ya kuwavutia wanafunzi wa vyuo vya kiufundi na vikuu.
Kwa kweli, sifa hizi zinastahili kuwa siri kuu. Tudor, Bangladesh, Mtwapa, Bomu na Magongo pia hakukosi vioja.
#MyLifestyle