Mkuu wa polisi katika kaunti ndogo ya Likoni mjini Mombasa Willy Simba amewataka abiria wanaotumia kivuko cha Ferry ya Likoni kuzingatia sheria zilizowekwa na shirika la huduma za Ferry ili kuepukana na maafa.
Simba ametaja hatua ya baadhi ya abiria kukaidi agizo linalowataka kushuka kwenye gari wanapovuka Ferry kama inayohatarisha maisha yao iwapo kutatokea ajali.
‘’Sheria inasema kuwa ukiwa ndani ya gari ukifika kwenye kivuko hichi unafaa kushuka uvuke ndio upande gari tena lakini wengine wenu mnakaidi mkijua wazi kuwa mnajiweka kwenye hatari iwapo kutatokea,’’ alisisitiza Simba.
Simba alikuwa akizungumza katika kivuko cha ferry mapema siku ya Alhamisi ambapo basi moja lililokuwa likielekea Tanzania lilitumbukia kwenye bahari baadaa kupoteza mwelekeo kufuatia breki zake kufeli japo hakuna mtu yeyote aliyeripotiwa kujeruhia.