Naibu Gavana wa Kwale Fatuma Achani katika hafla ya awali. [Picha/ nation.co.ke]
Naibu Gavana wa Kaunti ya Kwale ametangaza kuwania kiti cha ugavana katika uchaguzi wa mwaka 2022.Akihutubia mkutano wa wanawake wanaounga mkono chama cha Jubilee huko Matuga, Fatuma Achani alisema kuwa ana uwezo wa kushinda kiti hicho, na kuwataka wanawake wenzake kumuunga mkono kufanikisha malengo yake.Achani alisema ana imani atakuwa gavana wa kwanza wa kike Kaunti ya Kwale na katika eneo la Pwani kwa jumla.“Nina imani nitashinda kiti cha ugavana ifikapo mwaka 2022 na nitakuwa gavana wa kwanza wa kike eneo la Pwani,” alisema Achani.Achani alisema kwa muda mrefu wanawake wamekuwa wakiunga mkono viongozi wanaume, hali aliyosema imewasababisha wanawake kubaki nyuma kwa masuala ya uongozi.“Kwa miaka mingi wanawake tumetumiwa na wanaume kwa maswala ya kisiasa. Sasa wakati ni wetu wa kuwa viongozi,” alisema Achoki.Achani amewataka wanawake kuungana na kuchagua viongozi wa kike ili malengo ya wanawake yafanikishwe kwa haraka.Kauli yake iliungwa mkono na Spika wa Kaunti ya Nairobi Beatrice Alachi aliyempigia debe Achani kwa kumtaja kama mwanamke mkakamavu na mwenye msimamo dhabiti."Achani ni mama mchapa kazi ambaye haogopi vitisho. Tumchague kama gavana katika uchaguzi wa 2022,” alisema Alachi.