Afisa wa elimu katika divisheni ya Getembe wilayani Kisii ya Kati Ruben Migiro amewaomba walimu wakuu wa shule za msingi na za upili kutowadhulumu wanafunzi walemavu.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Akiongea afisini mwake na waandishi wa habari mnamo siku ya Jumatano, afisa huyo aliwaomba walimu wakuu wa shule kuwachukuwa wanafunzi walemavu kama wengine kwani nao ni binadamu kama wengine.

“Kila mwalimu mkuu wa shule ziko katika eneo la Kisii naomba kutowaona wanafunzi walemavu kama ambao hawahitajiki na kukubalika katika jamii na kuwachukuwa kama binadamu mwingine,” alidokeza Migiro.

Afisa huyo ambaye pia ni mlemavu amekuwa na utendakazi mwema, huku eneo hilo likinawiri katika mtihani wa darasa la nane na kuongoza katia kaunti ya Kisii, Nyamira na kaunti ya Migori.

Aidha, afisa huyo aliwaomba walemavu kutoombaomba katika mitaa ya mji wa Kisii, na kuwaomba kujifunza cha kufanya kwani mtu akiwa mlemavu sio mwisho wa maisha, na kuwaomba kujifunza kushona viatu, nguo na mafunzo mengine ili wajiendeleze kimaisha.

“Hawa wa kuombaomba kandokando mwa barabara za eneo la Kisii naomba wajifunze kwa ushonaji maana watajisaidi kwani wataomba mpaka lini, nasema huo ni uzembe ambao hauwezi saidia jamii ya mkisii, wakijifunza chochote cha kufanya wataendela na wakuwe matajiri,” aliongezea Migiro.