Shughuli ya usajili wa makurutu kujiunga na idara ya magereza iliongoa vyema kote nchini huku Nakuru ikishuhudia idadi ndogo katika uwanja wa Afraha.
Akizungumza na mwanahabari huyu katika uwanja huo wa Afraha, afisa wa Magereza Nakuru James Sawe alisema kuwa ni jambo la kusikitisha kwamba kando zoezi hilo kutangazwa katika vyombo vya habari, ina idadi ndogo sana ya vijana waliojitokeza.
Aliongeza kuwa huenda wananchi hawachukulii Kwa uzito idara ya magereza kando na marekebisho yaliyopo.
Ni kutokana na hilo ambapo alitoa wito Kwa vijana kukumbatia idara ya magereza na hata kujiunga nayo.
"Wito wangu Kwa wananchi ni kukumbatia zoezi kama hili na kuhakikisha wanajiunga na idara ya magereza manake Kwa sasa kuna Marekebisho kabambe katika idara hiyo,"alisema Sawe.
Wakati huo huo alitoa ushauri wake Kwa vijana kutokufa moyo maishani.
"Vijana hawafai kufa moyo wanapokosa kufaulu katika zoezi kama hili, manake si mwisho wa maisha," alisema Sawe.
Afisa Huyo alikuwa akizungumza ugani Afraha wakati wa shughuli ya kuwasajili makurutu wa kujiunga na idara ya Magereza.