Afisi ya mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma imepewa muda wa siku saba kukata rufaa kupinga kuachiliwa kwa Haniya Saggar, mjane wa Sheikh Aboud Rogo.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Saggar anadaiwa kukosa kutoa habari kwa polisi kuhusu uvamizi wa Kituo cha polisi cha Central, mjini Mombasa.

Hii ni baada ya mahakama kuu kutupilia mbali ombi la awali la kusimamisha dhamana ya shilingi milioni moja, lililowasilishwa na afisi ya mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma.

Akitoa uamuzi huo, Jaji Dora Chepkwonyi amesema Saggar aatachiliwa kwa dhamana aliyopewa, iwapo afisi ya mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma itakosa kukata rufaa.

“Iwapo siku saba zitapita basi mshukiwa huyo aachiliwe kwa dhamana,” alisema Jaji Chepkwonyi.

Jaji Chepkwonyi amesisitiza kamwe hawezi kupinga uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Shanzu kuhusu dhamana hiyo.

“Mahakama ya Shanzu ilitekeleza jukumu lake kikataba, na siwezi kuingilia uamuzi huo kamwe,” alisema Jaji Chepkwonyi.