Jengo la Mahakama ya Mombasa. [Picha/ the-star.co.ke]

Share news tips with us here at Hivisasa

Afisi ya mkurungenzi mkuu wa mashtaka ya umma imekata rufaa kupinga kuachiliwa huru kwa raia wawili wa India wanaokabiliwa na mashtaka ya ulanguzi wa dawa za kulevya.Praveen Nair na Vikas Balwan ni kati ya washukiwa 12 waliotiwa mbaroni kuhusiana na meli ya MV Darya iliyolipuliwa baharini na serikali.Washukiwa hao wanadaiwa kupatikana na heroine yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni moja kati ya Julai 7 na Julai 18 mwaka 2014 katika Bandari ya Mombasa.Akizungumza siku ya Jumatatu, naibu mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma tawi la Mombasa Alexendra Muteti amesema kuwa mahakama ya chini ilikiuka katiba kwa kuwaachilia huru wawili hao, ikizingatiwa ushahidi mwafaka dhidi yao uliwasilishwa mahakamani.Muteti alisema kuwa iwapo wawili hao wataachiliwa huru kabla ya kesi hiyo kukamilika, basi itakuwa vigumu kwa polisi kuwatia mbaroni washukiwa hao siku za mbeleni.“Itakuwa vigumu kwa polisi kuwapata wawili hawa iwapo wataachiliwa. Ni heri wazuiliwe korokoroni hadi rufaa hii ikamilike,” alisema Muteti.Hata hivyo, wakili wa washtakiwa Pascal Nabwana amepinga rufaa hiyo na kuitaja kama njama ya upande wa mashtaka kutaka kukandamiza haki za wateja wake.“Huu ni ukiukaji mkubwa wa haki za washtakiwa kwa mujibu wa katiba. Wateja wangu wanakandamizwa kwa vile wao sio raia wa Kenya,” alisema Nabwana.Wiki iliyopita, Hakimu Julius Nange’a aliwaachilia huru wawili hao kwa kuwa walikuwa wanafunzi waliokuwa wakipokea mafunzo ndani ya meli hiyo.Nange’a alisema kuwa wawili hao hawana ufahamu wowote kuhusiana na dawa za kulevya zinazodaiwa kupatikana kwenye meli hiyo.Meli hiyo ilizamishwa baharini na serikali mwezi Agosti 29, 2014 baada ya Rais Uhuru Kenyatta kutoa agizo la kuchomwa kwa meli hiyo.