Afueni kwa wakaazi wa Kaunti ya Uasin Gishu haswa mjini Eldoret baada ya bei ya nyanya kupungua kwa asilimia 28 kwa takriban wiki tatu.

Share news tips with us here at Hivisasa

Mwezi uliopita bei ya nyanya kwa kreti moja ilikua Sh2,500 lakini kwa sasa inauzwa kwa Sh1,800.

Kulingana na Peter Simiyu, mmoja wa wachuuzi katiika soko kuu mjini Eldoret chanzo cha kupungua kwa bei hiyo ni kuongezeka kwa nyanya kwani huu ni msimu wa kuvuna.

Aidha, jua inayozidi kuwaka inasababisha mmea huo kunyauka kwa haraka na kuambukiza ugonjwa unaosababisha nyanya kuoza kwa haraka pindi inapofika sokoni. Halikadhalika, bei ya bidhaa kama mboga ya kabeji na sukuma wiki na tikitiki maji kupanda.

Kwa mahojiano na ripota huyu Monicah, ambaye ni mchuuzi wa kabeji katika soko hilo, alielezea kwamba kabeji imekua nadra na inakosekana sana. Mboga hiyo sasa imepanda kwa asilimia hamsini na tano bei ambayo hawakutarajia ingefika hapo awali.

Alihoji kwamba kwa kawaida mmea huo hupatikana sehemu za Iten na Flax katika Kaunti ya Elgeyo Marakwet lakini wanalazimika sasa kusafiri hadi Meru na Molo kutafuta kabeji sababu ambayo imechangia kupanda kwa bei hiyo.

Mzazi huyo ambaye amekua kwa biashara hiyo kwa muda wa miaka saba sasa aliwasihi wanabiashara wengine kama yeye wasife moyo kwani misimu hubadilika kulingana na wakati.

Vile vile, aliwahimiza wanunuzi kuvumilia na kununua bidhaa hiyo kwa bei hiyo hadi msimu utakapowaruhusu kupunguza bei.