Serikali ya Kaunti ya Nyamira iliandaa mkutano ya vijana kutoka Kaunti hiyo ili kujua yale vijana wanahitaji kuwafanyia  na Serikali ya Kaunti ili kujiendeleza kimaisha na kimaendeleo.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mkutano huo wa vijana almaarufu Youth Forum uliandaliwa siku ya Ijumaa katika uwanja wa Uhuru Gardens katika mji wa Nyamira huku mgeni wa heshima akiwa afisa mkuu wa Wizara ya Vijana katika Kaunti hiyo Fridah Nyaboga.

“Tuliandaa mkutano huu ili tujue yale vijana wetu wanahitaji Serikali ya Kaunti yetu ya Nyamira iwafanyie ili wajiendeleze na kufurahia matunda ya ugatuzi,” alisema Nyaboga.

Wakati huo huo, Nyaboga aliwaomba vijana wa Kaunti hiyo kuunda vikundi mbalimbali ili waweze kujiendeleza kimaendeleo huku akisema vijana ni wengi wamesoma katika Kaunti hiyo lakini hawana ajira na kuwataka waungane pamoja na kupitisha ni lipi wangependa kufanya kwa kikundi husika.

Aidha, afisa huyo alitumia mfano wa kufuga Nyuki huku akiwaimiza vijana hao kuunda vikundi vingine na kuchagua mradi ambao wangependa kushughulikia.

Nyaboga, alisema kuunda vikundi kwa vijana itakuwa ni njia mojawapo ya kutambua ni lipi vijana watajiusisha nalo na kujua kiasi cha pesa Serikali ya Kaunti hiyo itawakabidhi.

“Tutawakabidhi pesa za mikopo punde tu mtakapounda vikundi na kuchagua miradi ya kufanya ili pesa hizo ziwasaidie kwa miradi hiyo,” alisema afisa Nyaboga.

Vile vile baadhi ya vijana wa Kaunti hiyo walifurahia hatua hiyo Serikali ilichukua na kusema wamesubiri kwa muda sana kukumbukwa kama vijana lakini yote yametimia huku wakisema watajaribu wawezalo kujiinua kimaisha baada ya kupokezwa mikopo hiyo na kuweka mikakati husika ya kufanya.

“Ninaomba vijana wote kuitikia wito huu na kujiunga kwa vikundi vya aina hii kwa kuwa hii ndio njia moja tunaweza saidika na Serikali ya Kaunti na kujiendeleza kimaendeo,” alisema Gerison Momanyi mmoja wa vijana kutoka Kaunti ya Nyamira.