Mwakilishi wa wanawake katika kaunti ya Kilifi Aisha Jumwa amewaonya wakaazi wa eneo la Pwani kukoma kudanganywa na viongozi wa kisiasa na siasa zao za kileo ili kuwachagua pindi uchaguzi mkuu ujao utakapowadia.

Share news tips with us here at Hivisasa

Jumwa amesema kuwa iwapo Wapwani wanahitaji maendeleo mashinani na kufanikishwa kwa maswala ya demokrasia basi lazima wawemakini katika kufanya uamuzi wa kuwachaguzi viongozi watakaowawakilisha katika maswala mbalimbali ya uongozi nchini.

Akionekana kumkosoa mbunge wa Kilifi Kaskazini Gideon Mung’aro, mwakilishi huyo wa wanawake kaunti ya Kilifi amesema kuwa viongozi kama hao waliyokosa kuungana na viongozi wenzao wameonyesha wazi kuwa sio viongozi waadilifu na hawafai kuchaguliwa.

Amesema kuwa wakaazi wanafaa kuwa macho kwani viongozi wengi ni watapeli na kamwe hawana malengo ya kuwasaidia wakaazi wa mashinani huku akishikilia kuwa viongozi wanaofaa kuchaguliwa ni kama yeye kwani anajali maslahi ya wananchi.

“Ningependa kuwaambia wakaazi wa Pwani chagueni viongozi wachapa kazi kama mimi kwa sababu wengi wa viongozi mnaowachagua wanamalengo potovu na kamwe hawajali maslahi ya wananchi, sini hata nyinyi muliwaona wengine walijitoa kwa chama chetu cha ODM sasa wanahangaika hao sio viongozi,” alisema Aisha mjini Mombasa siku ya Jumatatu katika mkutano wa wanawake kuhusu maswala ya maendeleo.

Kauli ya Kiongozi huo wa wanawake imejiri huku wakenya wakijiandaa katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka wa 2017 kuchagua viongozi watakaowafanyia maswala muhimu ya maendeleo mashinani.