Mwandishi Catherine Nandasaba Kulishuhudiwa ajali katika maeneo ya elementaita kwenye barabara ya Nakuru kwenda jogoo jumamosi mwendo wa asubuhi iliyohusisha matatu ya uchukuzi ya kubeba abiria kadri ya kumi na wanne Waliyoshuhudia ajali hiyo walisema kwamba dereva wa matatu hiyo aina SOLAl LINE alipoteza mwelekeo na kuishia kugonga kando mwa barabara baada ya kurudumu moja la gari hilo upande wa dereva kuisha pumzi Wakithibitisha ajali hiyo polisi kutoka katika kituo cha polisi cha elementaita wamewasihi madereva kuwa waangalifu na kutopuuza mambo madogo madogo kama ya pumzi kwenye makurudumu ya magari kuisha ili kuepuka visa ka hivyo na pia waliwarai madereva kuzingatia sheria zilizoekwa za barabarani Hadi kufikia wakati huo hakuna aliyeripotiwa kuaga dunia hali manusura walisaidiwa na wasamaria na walipelekwa kwenye hosipitali kuu ya mjini Nakuru huku dereva wa matatu hiyo wakionekana kukosa fahamu kwa kupata majeraha zaidi wakiwemo abiria sita huku abiria wengine na makanga wa gari hilo wakipokea majeraha madogo madogo Kila mmoja wetu anapaswa kuchukua jukumu la kuwaripoti madereva na wahudumu wa barabara wanapowaona hawazingatii sheria zilizoekwa za barabarani au wanapuuza mambo madogo madogo kama ya kurudumu la gari kuisha pumzi ili kupunguza visa vya ajali vinavyoripotiwa kila kuchao.
NAKURU
Ajali maeneo ya elementaita kwenye barabara ya Nakuru kwenda jogoo
ADVERTISEMENT
Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know
Thank you for reading my article! You have contributed to my success as a writer. The articles you choose to read on Hivisasa help shape the content we offer.
-Catherine Nandasaba