Shughuli za usafiri kwenye barabara ya Mai Mahiu-Nairobi zilitatizika mapema Jumatano kufuatia msongamano wa magari uliodumu kwa saa sita.

Share news tips with us here at Hivisasa

Katika kile kinachoonekana kuwa jambo la kawaida, wasafiri waliokuwa wakitumia barabara hiyo walilazimika kutafuta mbinu mbadala ili kuendelea na safari zao.

Hii ni mara ya pili katika kipindi cha wiki moja; malori mawili ya kubeba mzigo yalihusika kwenye ajali na kuifunga barabara hiyo, tukio lililopelekea msongamano huo.

Madereva sasa wamelaumu msongamano huo wa kila mara kwa muundo wa barabara hiyo na sasa wametaka ipanuliwe.

Mkazi mmoja, Joseph Njoroge, alisema kuwa; “Lori moja lilikuwa likielekea upande wa Mai Mahiu na lingine upande wa Nairobi wakati yalisababisha ajali hii lakini hakuna aliyeruhiwa.”

Polisi kutoka kituo cha Mai Mahiu baadaye walifika katika eneo hilo na kuondoa malori hayo huku hali ya kawaida ikirejea.