Idara ya trafiki kanda ya Pwani imekiri kuwa idadi ya ajali barabarani zimepungua katika eneo la Pwani mwaka huu ikilinganishwa na mwaka jana.
Akizungumza na mwanahabari huyu siku ya Jumamosi, mkuu wa idara ya trafiki kanda ya Pwani, Emmanuel Okanda, ametaja kupungua kwa ajali hizo ni kunatokana na juhudi za maafisa wa trafiki kupiga doria barabarani, kuhakikisha usafiri uko shwari na madereva kutoendesha kwa mwendo wa kasi.
Aidha, aliongeza kuwa kuondolewa kwa magari makukuu kumepunguza pakubwa ajali barabarani.
Okanda, amewataka madereva kuwa makini hasa wanapokuwa barabarani ili kuepuka ajali.
Wakati uo huo ameitaka idara husika inayoshughulikia maswala ya ukarabati wa barabara kufanya ukarabati wa barabara eneo la Pwani ambazo ameutaka kupunguza ajali katika eneo la Pwani.