Polisi katika eneo la Mumbuni wanaendelea kuchunguza kisa cha mwanamke wa umri wa miaka tisini na miwili aliyepatikana amejitia kitanzi katika eneo la Mukune, kata ndogo ya Kasinga. 

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Kwa mujibu wa naibu wa chifu wa Kasinga Robin Wambua ni kuwa ajuza huyo aliishi na familia yake pale alisubiri kila mtu kuondoka nyumbani kisha kujitoa uhai. 

Wambua alisema kuwa kilichomsukumia mwanamke huyo kujitoa uhai bado hakijabainishwa lakini polisi wameanzisha uchunguzi. 

Aidha, Wambua alisema kuwa kwa mujibu wa familia ya mwanamke huyo ni kuwa ilipigwa na butwaa kupata mwili wa ajuza huyo ukining'inia kutoka mtini mmoja uliopo nyuma ya nyumba yake. 

Aliwataka wenyeji kufunguka moyo wakati wamekumbwa na shida na kuzungumza na familia zao, wahubiri au wataalamu wa kutoa mawaidha ili kupata suluhisho.

"Si vyema mtu kukadiria kujitoa uhai wakati amekumbwa na matatizo wakati kuna watu wengi walio tayari kuwasikiliza na kuwashauri, " alisema Wambua. 

Mwili wa mwanamke huyo ulipelekwa katika hifadhi ya maiti ya hospitali ya Machakos level five.