Ajuza mwenye umri wa takriban miaka 70 amefikishwa mahakamani kwa kosa la kupatikana na pombe haramu aina ya chang’aa.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Paulina Nabwire, alipatikana na lita 70 za pombe katika eneo la Mikindani siku ya Jumatano.

Nabwire alijitetea mbele ya Hakimu Teresia Matheka kwa kusema kuwa pombe hiyo ndio pato lake la kupata pesa za kukimu mahitaji yake ya familia na kuweza kusomesha wajukuu wake.

“Sina kazi wala bwana. Nafanya biashara hii ili kusomesha wajukuu wangu,” alisema Nabwire.

Ajuza huyo ameachiliwa kwa dhamana ya Sh40,000 ama kifungo cha miezi sita gerezani.