Huku serikali na washikadau wakiendelea kubuni njia za kuboresha viwango vya eimu nchini, kutowajibika kwa baadhi ya wazazi kum kama mojawapo ya mambo yanayotishia elimu ya watoto wasichana kaunti ya Kisii.
Hayo yalisemwa siku ya Jumatatu katika mazishi ya mwenda zake Swanya Birundu aliyekuwa mfanyakazi katika Wizara ya Ardhi kutoka eneo la Gesusu Masaba.
Akiongea siku hiyo, bwana Evans Kalulu, Mwekahazina wa chama cha walimu (Knut) eneo la Masaba Kusini alidai kuwa akina mama wakiwa ndio wametwikwa jukumu la kuwaelimisha watoto wasichana wamezembea na ndiyo maana wasichana wengi katika eneo hilo hukosa kukamilisha masomo yao.
"Wasichana wengi hawakamilishi masomo ya shule ya msingi ambayo hayalipiwi na ni ya lazima kwa watoto wetu. Wazazi wao wanafaa kushitakiwa na serikali kisheria. Nawaomba, kabla hatua hiyo haijachukuliwa dhidi yenu hakikisheni watoto wenu wako shuleni mara moja," alionya Kalulu.
Aidha amewakosoa wazazi wa kiume kwa kutofuatilia masomo ya mtoto msichana na kuhakikisha amepata nafasi sawa kama wenzao wa kiume akionya kuwa kukosa kumpa elimu mtoto msichana ni tishio kwa maendeleo eneo hilo na kuwataka wazazi kuwajibika.
Pia swala hilo lilisungumziwa na wanasiasa wa eneo hilo na kuahidi kushirikiana na maafisa wa elimu pamoja na wazazi ili kuhakikisha wasichana wamepewa nafasi ya kipekee katika nyancha mbalimbali za kimaendeleo na kujiendeleza kimaisha sawa na watoto wa kiume katika jamii ya Wakisii.
Mwanasiasa mbaye ametangaza nia yake ya kuwania kiti cha ubunge Nyaribari Masaba, Bernard Moseti, ameahidi kushirikiana na wakaasi hao hili kuimarisha masomo yao.