Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mwenyekiti wa chama cha maendeleo ya wanawake katika Kaunti ya Kisii Patishebah Sanaya amewalaumu baadhi ya makundi hayo kutumia pesa za Uwezo Fund kwa kupika pombe badala ya biashara tofauti.

Hii ni baada ya kupokezwa habari hiyo kutoka kwa watu fulani ambao wanadai kujua baadhi ya vikundi ambavyo vilipokezwa pesa za uwezo fund kufanyia biashara tofauti na kuzibadilisha na kufanyia biashara ya kupika pombe ambayo ni kunyune na sheria za hapa nchini.

Habari hii imeibuka wakati pombe ilikuwa inamwagwa sehemu za Kisii huku wenye pombe hiyo wakipiga mayowe kuwa wamepata hasara kwani pesa ni za Uwezo Fund ambazo na zinahitajika kurudishwa kwa hazina ya serikali pamoja na faida.

Akiongea siku ya Ijumaa katika sherehe ya mazishi katika sehemu ya Igare, eneo bunge la Bobasi katika Kaunti ya Kisii, Sanaya alisema hajafurahishwa na habari hiyo ya kutumia pesa za Uwezo Fund kupika pombe haramu.

“Nawaomba akina mama wenzangu wakome tabia ya kupika pombe na kufanya biashara mbadala kwani pombe ni biashara haramu,” alisema Sanaya, mwenyekiti wa chama cha akina mama Kaunti ya Kisii.

Wakati uo huo, Mbunge wa Bobasi iliyoko Kaunti ya Kisii Steve Manoti aliomba watu kutopika pombe na kufanya biashara tofauti ili kukwepa kusakwa na polisi.

“Pombe haitusaidi na inaathiri vijana wetu na hata kuvunja ndoa nyingi. Kwa hiyo nawasihi muachane na na mambo ya pombe haramu,” alisema Mbunge Manoti.