Msanii wa Kenya aliye na makaazi yake hapa Mombasa Esther Akoth maarufu kama Akothee, ameendelea kuchukua vichwa vya habari katika tasnia ya muziki si hapa nchini tu bali pia Afrika mashariki, hii ni baada ya kuonyesha picha zake za harusi akiwa na mpenzi wake bwenyenye raia ya Swaziland.
Muimbaji huyo alijisifia kuwa weusi wake ndio kitu kilichompendezea bwanake, kinyume na wasichana wengi nchini, wengi hujichubua kwa kutumia kemikali ili kubadilisha rangi ya mwili.
Nyota huyo wa my 'Sweet love' aliendelea kusema kuwa licha ya kuwa tayari ana watoto watano, mpenzi wake amemkubali na sasa amemakribisha rasmi katika familia yake.
Aidha, alishindwa kuficha furaha yake na kuidhihirisha wazi katika mtandao wa kijamii alipoandika kwa lugha ya kimombo.
‛‛Mimi ni mwanamke anayefanya kitu anachokitaka na wala sio kitu kiliopo, weusi wangu ndio kilichomvutia mpenzi wangu, mbali na kuwa mama wa watoto watano, mpenzi wangu ameridhika na mimi, na namkaribisha nyumbani ,’’ Akothee aliandika.
Pia hakusita kujigamba na ukwasi wa mali anayomiliki kwa sasa, huku mazingira aliyofunga harusi hiyo yakionesha utajiri wake, Akothe ni miongoni mwa wasanii wa kike matajiri zaidi katika ukanda wa Afrika mashariki.
Kwa sasa Akothee ni mjamzito na anatarajiwa kukaa kimya kwa mda mrefu kimziki hadi pale atakapojifungua.