Msanii Esther Akoth, al maarufu Akothee, ameibuka mshindi wa tuzo la African Muzik Magazine (Afrimma) 2016.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Licha ya kupoteza tuzo katika kitengo cha video bora ya mwaka, ambapo wimbo wake 'My Sweet Love' aliomshirikisha Diamond Platinumz ulikuwa umeteuliwa, Akothee aliibuka mshindi wa tuzo hizo katika kitengo cha msanii bora wa kike Afrika Mashariki.

Akothee alionyesha furaha tele na kuwashukuru mashabiki wake kwa kumuunga mkono.

Sauti Sol ambao pia walishinda tuzo la kundi bora Afrika, hawakusita kumpongeza Akothee kwa kuletea nchi ya Kenya sifa nzuri.

Hii ilikuwa historia kwani hakuna msanii kutoka ukanda wa Pwani ambaye amewahi kushinda tuzo hilo tangu kubuniwa kwake miaka mitatu iliyopita.

Akothee aliwabwaga wapinzani Victoria Kimani, Venessa Mdee, Linah Nguli, Tsedenia Gebremarkos, Esther Aweke, Knowles Butere na Sheebah Karungi, katika tuzo hilo lilioandaliwa jijni Dallas Texas, Marekani siku ya Jumamosi.