Akothee, msanii kutoka Mombasa amezua mjadala miongoni mwa mashabiki wake baada ya kutuma picha pamoja na ujumbe akisema kuwa ni mjamzito.
“Wacha tuone ni nani huyu anakosesha mama amani. Uliuliza nimeenda wapi hayaa, nimekuja clinic. Toto ya my king iko na sipesiol doctor,” aliandika msanii huyo kwa lugha ya utani katika mtandao wa kijamii.
Akothee huenda akakaa nje kwa muda baada ya kushauriwa na daktari kupumzika kwa zaidi ya miezi miwili.
Ujumbe huo umewaacha mashabiki wake katika njia panda, huku baadhi yao wakidai kuwa ujumbe huo huenda ukawa njia moja ya kuendelea kujiweka katika ramani ya muziki.
Akothee, ambaye ni mama wa watoto watano, kwa hivi sasa yupo nchini Afrika Kusini na alituma ujumbe huo akiwa katika hospitali ya Netcare Rosebank.
Akothee aliwashtua mashabiki wa mzuki wa kizazi kipya nchini kwa jinsi alivyopata umaarufu kwa haraka katika tasnia ya muziki, hasa baada ya kushirikiana na wasani tajika wakiwemo Diamond Platinumz na msani kutoka Nigeria Mr Flavour.
Msanii huyo anatarajiwa kuwa jiko la mpenzi wake bwenyenye raia wa Switzerland mwezi Novemba mwaka huu.