Ukanda wa Pwani unaendelea kuwakilishwa vyema katika tasnia ya muziki na Akothee, aliye na makazi yake jijini Mombasa.

Share news tips with us here at Hivisasa

Binti huyo ambae hivi karibuni ameibua mjadala katika vyombo vya habari kuwa huenda akahamia ughaibuni na barafu wake wa moyo ni miongoni mwa wasanii walioteuliwa kushiriki tuzo za Afrimama katika vitengo viwili tofauti.

Akothee anatarajia ushindani mkali kutoka kwa wasanii kama vile Phyno, Olamide, Pantoranking na wengineo.

Ameteuliwa katika kitengo cha mwanamuziki bora wa kike kutoka Afrika Mashariki, na kitengo cha video ya mwaka kupitia wimbo wake My Sweet Love, aliyomshirikisha nyota wa Tanzania Nassib Abdull al maarufu kama Diamond Platinumz.

Licha ya mashabiki na washika dau katika tasnia ya muziki kukejeli jinsi anvyoendesha miasha yake binafsi, Akothee anendelea kuwa kio cha jamii kwa wasanii wakongwe na chipukizi kutoka kanda ya Pwani.

Ujio wake katika tasnia ya muziki haujachukua muda mrefu bila mafanikio kujitokeza.

Wanamziki wengine walioteuliwa katika tuzo hizo vitengo tofauti kutoka hapa nchini ni pamoja na kundi la Sauti Sol, Victoria Kimani, Octopizzo na King Kaka, miongoni mwa wasani wengine.