Wanamgambo wa kundi la al-Shabaab. [Picha/ hiiraan.com]

Share news tips with us here at Hivisasa

Kamanda wa oparesheni ya Linda Boni James Seriani amesema kuwa visa vya vijana waliojiunga na kundi la al-Shabaab kuuawa vinazidi kuongezeka.Seriani alisema kuwa vijana hao wanauawa na wanamgambo hao katika njia ya kutatanisha kwa kushukiwa kuwa majasusi wa serikali ya Kenya.Akizungumuza na wanahabari mjini Lamu, kamanda huyo alisema takriban vijana sita wameuawa huko Somalia na kundi hilo haramu kati ya mwezi Machi na Aprili mwaka huu.Hata hivyo, Seriani alisema kuwa wao kama idara ya usalama humu nchini hawataruhusu visa hivyo kutekelezwa.Aidha, alisema kuwa tayari kuna baadhi ya vijana waliofanikiwa kutoroka na kurudi humu nchini.Seriani alisema kuwa vijana hao wamejisalimisha kwa idara ya usalama na watapata fursa ya kujumuika na familia zao na pia kupewa usalama kama wananchi wa kawaida.Wakati huo huo, amewataka maafisa wa usalama kutowahangaisha vijana katika kazi zao na kuomba ushirikiano na wananchi ili kuboresha usalama katika eneo la Pwani.