Handa katika hafla ya awali. Picha/ citizentv.co.ke
Aliyekuwa difenda wa klabu ya Gor Mahia, Re Union FC na klabu ya Coast Stars Charles 'Sodja' Handas ameaga dunia.
Handas alifariki siku ya Jumanne jioni katika hospitali ya Nairobi West alikokuwa akipokea matibabu.Handas amekuwa akiugua uvimbe wa damu katika ubongo.Baada ya kutamatisha hatamu yake kama mchezaji, Handas alijiunga na safu ya uamuzi na kuwa kama mpuliza kipenga.Wadau mbali mbali wa soka nchini wametoa risala zao za rambi rambi kwa familia ya marehemu akiwemo mwenyekiti wa chama cha wakufunzi nchini Kenya Ricky Solomon.