Aliyekuwa mwakilishi wa wadi ya Jomvu Kuu Karisa Nzai. [Photo/ the-star.co.ke]
Mahakama ya Mombasa imemuachilia huru aliyekuwa mwakilishi wa wadi ya Jomvu Kuu Karisa Nzai.Nzai alikuwa amehukumiwa kifungo cha mwezi mmoja gerezani kwa kosa la kushindwa kulipa deni la zaidi ya shilingi milioni moja.Kampuni ya Javaco Agencies Limited inamdai Nzai shilingi1,464,255 ambazo alikuwa amekopa kutoka kampuni hiyo.Nzai amepewa makataa ya siku14 kulipa kampuni hiyo shilingi laki tano au aregeshwe gerezani.Akitoa uamuzi huo siku ya Jumatatu, Hakimu Francis Kyambia pia alimuagiza Nzai kulipa shilingi laki mbili kila mwezi hadi pale atakapomaliza kulipa deni hilo.Wiki iliyopita, Hakimu Kyambia alimhukumu Nzai kutumikia kifungo cha siku 30 gerezani baada ya kukiuka agizo la mahakama la kulipa deni hilo.Nzai ambaye aliwania kiti cha ubunge Jomvu katika uchaguzi wa Agosti 8, alitiwa mbaroni siku ya Alhamisi wiki iliyopita akiwa katika nje ya jengo la mahakama.Agizo hilo la Nzai kutiwa mbaroni lilitoloewa tarehe Juni 6, 2017.