Aliyekuwa mwakilishi wa wadi ya Jomvu Kuu Karisa Nzai katika hafla ya awali. [Photo/ the-star.co.ke]
Aliyekuwa mgombea wa kiti cha ubunge eneo la Jomvu Karisa Nzai amehukumiwa kifungo cha siku 30 jela kwa kosa la kushindwa kulipa deni la Sh1,464,255.Nzai, ambaye pia alikuwa mwakilishi wa wadi ya Jomvu kuu, anadaiwa pesa hizo na kampuni ya Javaco Agencies Limited, iliyoko jijini Mombasa.Akitoa uamuzi huo siku ya Alhamisi, Hakimu Francis Kyambia alisema kuwa Nzai amekiuka agizo la mahakama la kulipa pesa hizo kwa muda sasa.“Nzai amekiuka agizo la mahakama la kumtaka kulipa pesa hizo kama alivyosema mbele ya mahakama hii,” alisema Hakimu Kyambia.Aidha, Kyambia ameagiza wasimamizi wa gereza la Shimo la Tewa kutomuachilia mwanasiasa huyo hadi atakapomaliza kifungo hicho au atakapolipa lipa deni hilo.“Musimuachilie hadi atakapomaliza kutumikia kifungo hicho cha siku 30 ama atakapolipa deni analodaiwa,” alisema Kyambia.Nzai alitiwa mbaroni siku ya Alhamisi akiwa nje ya jengo la mahakama.Agizo hilo la kutiwa mbaroni lilitoloewa tarehe Juni 6, 2017.