Aliyekuwa naibu mhadhiri mkuu wa Chuo kikuu cha kiufundi cha Mombasa TUM, Profesa Awadh Binhazim na wafanyikazi wengine watano wameachiliwa kwa dhamana ya shilingi elfu 50 kwa kosa la utumizi mbaya wa afisi.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Profesa Binhazim, Gaireth Kingi Feiruz, Jumaa Kaloo, Joseph Obwagi, Titus Tunje na Ernest Makhulo wanadaiwa kununua televisheni yenye thamani ya shilingi milioni 4.7 mnamo Septemba 22, 2015.

Washukiwa hao walikanusha madai hayo mbele ya Hakimu Douglas Ogoti siku ya Jumatatu.

Kesi hiyo itasikizwa tena tarehe Agosti 16, 2016.