Share news tips with us here at Hivisasa

Baadhi ya wanasiasa Pwani wametaka Mbunge wa Lamu Magharibi Julius Ndegwa kuchukuliwa hatua za kisheria kwa madai ya kutoa matamshi ya uchochezi.

Katika kikao na wahabari afisni mwake jijini Mombasa siku ya Jumatano, Naibu mwenyekiti wa kitaifa wa chama DP, Rishad Amana, alisema kuwa kauli kama hiyo kutoka kwa kiongozi haifai ikizingatiwa hali ya usalama ilivyo katika eneo hilo kwa sasa.

Amana alisema kuwa wakazi katika Kaunti ya Lamu wanaishi vyema na jamii kutoka kaunti zingine jirani kama vile Tana River, na kauli kama hiyo huenda ikaleta mtizamo tofauti.

Amana hata hivyo amewataka viongozi wakuu kutoka Kaunti ya Lamu kuwa kitu kimoja badala ya kutoa matamshi ambayo huenda yakaleta mtafaruku baina ya jamii kutoka eneo hilo na kaunti zengine jirani.

Ndegwa anadaiwa kusema kuwa wafugaji walioko katika Kaunti ya Lamu wanapswa kufurushwa kutoka eneo hilo kwa kisingizio cha kusabisha ukosefu wa usalama.

Jamii za wafugaji walioko huko Lamu wanatoka katika Kaunti za Tana River na Garissa na wanaendeleza shughuli zao katika maeneo ya Bodhei, Pandaguo, Witu miongini mwa maeneo mengine.

Kaunti ya Lamu imekuwa ikikumbwa na mashambulizi ya mara kwa mara kutoka kutoka kwa kundi linaloaminika kuwa al-Shabaab.