Wakazi wa eneo bunge la Kitutu Chache kaskazini kaunti ya Kisii  wamemwomba mbunge wa eneo hilo Jimmy Angwenyi kuikarabati barabara aliyoilima hapo awali ya kutoka Marani kuelekea eneo la Ngokoro.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wakizungumza na mwandishi huyu mnamo siku ya Ijumaa, wakazi hao walikiri kuwa mvua inayoendelea kunyesha imesababisha barabara hiyo kutopitika, jambo ambalo limewakera sana na kumwomba mbunge huyo kuweka mchanga haraka iwezekanavyo ili kuwezesha operesheni za kawaida. 

“Kila wakati mvua inaponyesha, gari haliwezi pita barabara hii hata sisi, wenyewe hatupiti, tunaomba mbunge wetu atuwekee mchanga tumalizane naye roho safi ili akamilishe shughuli aliyoianza hapo mapema,” alisema Cicilia Makori, mkazi wa eneo bunge hilo.

Inabainika kuwa barabara hiyo imekuwa ikisuwambua wakazi hao wanapopita haswa mvua inaponyesha na kusimamisha shughuli za uchukuzi katika eneo hilo kila wakati.

“Ikiwa mbunge wetu atafanya yale alituahidi jinsi tunahitaji kwa kulikarabati barabara hii ya Marani –Ngokoro, basi hatuna budi sisi ila kumrudisha kwenye kiti chake, na ikiwa anaanzisha mradi bila kukamilisha basi kura si kwake tena na hilo ni la ukweli,” alisema David Makworo.