Mbunge wa Kitutu Chache kaskazini kaunti ya Kisii Jimmy Angwenyi amewaomba wakaazi wa kaunti ya Kisii kumpa gavana wa kaunti hiyo James Ongwae mda zaidi ili kutimiza miradi aliyo nayo kwa kaunti yake.
Akizungumza siku ya Ijumaa katika uga wa shule ya upili ya wasichana na Marani iliyoko eneo bunge lake wakati wa hafla ya mazishi ya mfanyikazi wa mbunge huyo, mbunge huyo alisema kuna haja ya wakaazi kumpa gavana wakati mwafaka kutimiza miradi aliyo nayo katika kaunti ya Kisii.
“Gavana wetu James Ongwae yuko na miradi mingi ya kufanya, naomba mumpe mda kutimiza na kutekeleza ahadi ako nazo,” alisema Angwenyi.
“Msipompokeza wakati mwafaka, itakuwa vigumu kwake kutimiza ahadi zenu maana tayari amepanga miradi ya kushughulikia kama ujezi wa mahospitali, maji na ujenzi wa taasisi katika kaunti hii ya Kisii,” aliongeza Angwenyi.
Wakati huo huo, viongonzi waliohudhuria hafla hiyo kutoka kaunti ya Kisii walihapa kufanya kazi pamoja ili viwango vya maendeleo kuinuka zaidi.
Viongonzi waliohudhuria hafla hiyo ni gavana Ongwae, mbunge wa Kitutu Chache Kusini Richard Onyonka, Seneta mteule kaunti ya Kisii Hosea Onchwang’i, wawakilishi wa wadi mbalimbali za kaunti ya Kisii pamoja na wananchi wote kwa jumla.