Baada ya malalamishi kutoka kwa wakazi wa eneo bunge la Kitutu Chache kaskazini Kaunti ya Kisii, sasa wakazi hao wanamtaka mbunge wao Jimmy Angwenyi kuwaelezea bayana jinsi pesa za basari zilikuwa zinagawa katika eneo bunge hilo na ni mtindo upi ulikuwa unafuatwa.
Wakiongea na waandishi wa habari siku ya Jumanne mjini Marani, kiongozi wa vijana katika wadi ya Marani David Omwancha na wakazi wengine walisema hawajui jinsi pesa hizo zinagawa katika eneo bunge hilo.
Wakati huo huo, vijana hao wamedai baadhi ya vijana wa wadi zingine hufaidika na fedha hizo kando na sehemu zingine ambao wamejiendeleza kibiashara, huku wakishindwa chanzo cha sehemu zingine kama Marani, Nyakeiri, Sensi hutengwa
“Tunaomba kuelezwa na mbunge wetu jinsi pesa hugawa katika eneo bunge hili. Hatujui ni njia ipi huwa inatumika kwa ugavi, ndio tunamhitaji mbunge wetu ajitokeze wazi atuelezee,” alisema Omwancha.
Aidha, wakazi hao waliongezea kuwa idadi kubwa ya wanafunzi hutoka katika eneo hilo ambao wako katika vyuo vikuu na hawajawahi faidika na pesa za basari kujifadhili kimasomo.