Seneta wa kaunti ya Kisumu profesa Anyang Nyo’ngo amewataka wawakilishi wadi kufuata katiba na kukoma kusema kuwa hawataondoka afisini hadi Machi 2018.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akizungumza jijini Mombasa siku ya Jumatano kwenye kongamano la maseneta na wakilishi wadi, Nyo’ngo alisema ni lazima katiba iangaliwe kwa makini na kisha kufuatwa pasi kukiukwa.

Aliongeza kuwa katiba inaeleza wazi tarehe za uchaguzi ujao ishara tosha kuwa viongozi wote walioko madarakani watabanduka kabla uchaguzi mkuu ujao ili kupigiwa kura upya.

Aliyasema haya kufuatia kauli ya spika wa kaunti ya Tana River aliye pia mwenyekiti wa muungano wa mabunge ya kaunti nchini Abdi Nuh Nassir kuwa wawakilishi wote wa kaunti hawatoondoka ofisini hadi machi 2018.