Mbunge wa Nakuru Magharibi Samuel Arama ametoa wito kwa kiongozi wa mungano wa CORD Raila Odinga, kujitolea na kwenda kutoa ushahidi wa kumtetea naibu wa Rais William Ruto huko Hague.

Share news tips with us here at Hivisasa

Arama alisema kuwa iwapo Odinga atakubali wito huo basi itaonyesha kuwa hakuwa na ubaya na Ruto na pia hakuhusika kwa vyovyote vile katika kufikishwa kwa Ruto huko Hague.

Akiongea mjini Nakuru Alhamisi, Arama alisema kuwa itakuwa vyema iwapo Odinga atajitolea kwenda kumtetea Ruto kwa vile alikuwa akimuunga mkono na kumpigania baada ya uchaguzi wa mwaka 2007.

“Mimi nataka kumrai aliyekuwa waziri mkuu Bwana Raila Odinga, aende katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu dhidi ya binadamum, Hague na amtetee Ruto kwa vile alikuwa akimpigania wakati wa uchaguzi wa 2007,” alisema Arama.

“Kama anampenda Ruto na anataka Ruto arudi nyumbani basi aende na amtetee mbele ya korti hilo ili aachiliwe kwa kuwa Ruto hana makosa,” alisema Arama.

Arama alisema kuwa huu ni wakati mwafaka kwa Odinga kujitolea na kumsaidia Ruto kama njia ya kumshukuru kwa jinsi alivyosimama naye mwaka 2007.

“Jambo lililomfanya Ruto kupelekwa Hague in uchaguzi wa 2007 na kwa sababu alimfanyia Odinga kampeiniwakati huo kwanini Odinga asimsaidie,” alisema Arama

Mbunge huyo pia aliunga mkono kubuniwa kwa chama kipya kilicho unganisha mlengo wa jubilee.

“Hiki chama kitasaidia kuwaunganisha wakenya,” alisema Arama.