Kuna umuhimu wa wanafunzi kuelimishwa shuleni kuhusiana na athari za ufisadi kwa taiga kama njia mojawapo ya kumaliza ufisadi humu nchini.
Mbunge wa Nakuru mjini magharibi Samuel Arama katika mahojiano na mwanahabari huyu kwa njia ya simu Jumanne alisema kuwa hatua hiyo itasaidia pakubwa katika kuhakikisha watoto wanatambua athari za ufisadi.
Alisema kuwa kuna umuhimu vile vile wa mtaala wa elimu kujumuisha somo maalum kuhusu ufisadi na athari zake Kwa taifa.
"Tunajua ufisadi ni zaidi ya saratani katika taiga hili lakini tunaweza kuokoa kizazi kijacho kwa kuanza kuwafunza kuhusu athari za ufisadi kwa taifa hata katika shule za msingi," alisema Arama.
Wakati uo huo, alimpongeza waziri wa elimu Dkt Fred Matiang'i kwa kujaribu kuweka mikakati kabambe katika sekta ya elimu humu nchini.
Alisema kuwa kama wabunge, watazidi kuunga mkono mageuzi ya maana katika sekta ya elimu.