Share news tips with us here at Hivisasa

Mbunge wa Nakuru Mjini Magharibi Samuel Arama ameshtumu idara ya polisi kwa kuwanyanyasa wanawake wanaofanya biashara ya ukahaba mjini Nakuru.

Katika kikao na wanahabari mjini Nakuru siku ya Jumapili, Arama alisema kuwa wanawake hao hawafai kuhangaishwa pekee yao kwani hushiriki biashara hio na wanaume.

"Mi nashangaa kwa nini ni wanawake tu wanashikwa. Inafaa wanaume pia watiwe mbaroni kwasababu hao ndio huwa wateja wa wanawake hao,” alisema Arama.

Wakati huo huo, mbunge huyo alitoa wito kwa Gavana Kinuthia Mbugua kuingilia kati swala hilo la makahaba kuuawa kila mara mjini Nakuru.

Haya yanajiri huku kukiwa na msururu wa visa vya makahaba kuuawa humu nchini katika hali tatanishi.

Arama vilevile alitoa wito kwa vyombo vya habari kufanya uchunguzi wa kina kuhusiana na swala hilo.