Mbunge wa magharibi mwa Nakuru, Samuel Arama amesema kwamba mkutano uliofanyika kwenye uwanja wa Afraha Nakuru ni mwanzo mpya kwa siasa za Kenya na uongozi wa Jubilee. Ameendelea kusema kwamba mkutano huo utaipa nafasi Jubilee katika uongozi hadi mwaka wa 2032.

Share news tips with us here at Hivisasa

Ametoa wito kwa wapinzani wa Jubilee kufikiria upya kwani Jubilee itaongoza hadi Mola akatae.

“Jinsi watu walivyohudhuria mkutano huo inaonyesha kuamini kwao uongozi wa Jubilee. CORD inafaa kuwapa nafasi Jubilee hadi Mungu aseme imetosha kwa sababu Jubilee haitashindwa,” alisema Arama.

Arama aliwashauri Cord kususia uchaguzi wa mwaka wa 2017 ili kuepukana na aibu za kisiasa