Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Rais Uhuru Kenyatta amewaahidi wafanyibiashara wa kongowea Mombasa kuwa ardhi ya soko hiyo iliyonyakuliwa itaregeshwa.

Rais amesema atarudi Mombasa kwa ziara rasmi mwezi wa agosti kufungua ujenzi wa soko ili kutoa nafasi kwa wachuzi kupata mahali pa kuuzia bidhaa zao.

Wakati wa ziara yake hapo Jumanne katika soko hilo, Rais alisema kuwa haungi mkono ubomoaji wa maduka.

"Kiongozi wa kweli ni yule anayezingatia maswala ya watu wake, nitahakikisha kuwa kipande hiki cha adrhi kimeokolewa na kurejeshwa ili kutumika kama soko," alisema Rais.

Kuhusiana na suala la mirundiko ya taka sokoni humo, Rais alimwelekeza waziri wa utumishi wa umma Sicily Kariuki kutuma huduma kwa vijana NYS kusafisha soko hilo mapema mwezi ujao.