Maafisa wa Trafiki pamoja na Askari wa Kaunti ya Kisii wametwikwa lawama kufuatia hali isiyokuwa ya kawaida iliyoshuhudiwa katika barabara zote za kuingilia na za kutoka katika mji wa Kisii.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wakiongea na Mwandishi huyu siku ya Alhamisi jioni, baadhi ya wakaazi na wahudumu wa matatu ambao walikuwa wamekwama kwenye msongamano wa magari kwa zaidi ya saa mbili, waliwashtumu Maafisa hao kwa uzembe wanaposhughulikia masuala yanayomlenga mwananchi.

Charles Maina, dereva wa kampuni ya magari ya Mbukinya Travellers aligadhabishwa na utepetevu ulionyeshwa na Askari wa Kaunti hiyo akisema kuwa walikosa kuonyesha uwajibikaji wa kikazi na kuitaka Wizara ya Mipango na Uratibishaji wa mji kuwafundasha jinsi ya kuelekeza magari ili kupunguza msongamano wa magari ambayo imekuwa kero sana kwa wakaazi wa eneo hilo.

Kwa upande wake Jonhstone Mokua ambaye ni mwenyekiti wa Ziwani Matatu Sacco alionyesha kutoridhika kwake kuhusiana na msongamano huo ulioshuhudiwa siku ya Alhamisi ambapo aliwalaumu Mafisaa hao na kudai kuwa walikuwa wanapendea baadhi ya magari ya binafsi hasa wafanyakazi wa kaunti ambao walikuwa wanaruhusiwa kutumia njia mbadala ya RAM hospital ambayo ilichangia msongamano zaidi.

"Sharti Serikali ya Kaunti iwajibike vilivyo, si haki kufungulia wengine kutumia barabara fulani na kuacha wengine kwenye msongamano wa magari kwa muda wa saa mbili. Naomba Wizara husika kuangalia suala hili haraka iwezekanavyo,” alilalama mwenyekiti huyo.