Askofu Naftali Thuku wa kanisa la AIPCEA Nakuru ameunga mkono niya ya serikali ya kuzifunga kambi za wakimbizi japo ametaka sheria kufuatwa katika swala nzima.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Katika mahojiano ya kipekee mjini Nakuru, Askofu Thuku alisema kuwa ni jambo la busara kwa kambi hizo za Dadaad na Kakuma kufungwa hasua ikizingatiwa yale mambo ambayo yamekuwa yakitajwa kuendelezwa katika baadhi ya kambi hizo.

Hata hivyo, alitoa wito kwa viongozi kuhakikisha kwamba sheria inafuatwa katika swala nzima ili kuepuka madhara.

"Swala la wakimbizi na kufungwa kambi zao ni busara na mimi naunga mkono lakini ombi langu ni kwamba utaratibu wa kisheria ufuatwe katika swala nzima ili tusiwe na athari zozote," alisema skofu huyo.

Wakati huo huo alitoa wito kwa viongozi wa kisiasa kuhakikisha kwamba hawaingizi siasa katika maswala ya kufungwa kwa kambi hizo kwani kufungwa kwazo ni kwa manufaa ya taifa kwa jumla.

Haya yanajiri huku hisia mseto zikizidi kutolewa kuhusiana na swala nzima la wakimbizi na hatua ya serikali kutangaza kufungwa kambi hizo.