Askofu Mark Kariuki amesema kuwa Kenya ina mwamko mpya baada ya kesi za ICC kutamatika.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Akizungumza Jumamosi wakati wa hafla ya shukrani mjini Nakuru, Kariuki alisema kuwa Kenya ni taifa lenye baraka na mwamko mpya ni kuombeana, kusameheana na kuridhiana.

Alisema kuwa viongozi wanafaa kuhakikisha kila mwaathiriwa wa ghasia za baada ya uchaguzi anafidiwa na amani kudumishwa.

"Tumeanza mwamko mpya na ni jukumu la kila kiongozi kuhakikisha anahubiri amani,"alisema Kariuki.

Wakati huo huo, Kariuki aliyeongoza maombi hayo Kwa usaidizi wa viongozi wengine wa kidini alisisitiza kwamba taifa linalomheshimu Mungu hufaulu.

Alitoa wito kwa Rais Uhuru Kenyatta kuendelea kuwaunganisha wakenya hasa tunapokaribia uchaguzi mkuu.