Askofu wa kanisa la Evengelica Lutherlan tawi la Nyamira Thomas Obare amejitokeza kuwataka wakristo kote nchini kukumbatia amani na ukarimu ulimwengu unapotarajia kuadhimisha siku kuu ya pasaka ijumaa wiki hii. 

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Akihutubia waumini wa kanisa hilo tawi la Nyamira siku ya Jumapili, Obare alisema kwamba siku kuu ya pasaka ni ya umuhimu mkubwa kwa wakristo kote ulimwenguni kwa maana huo ni wakati mwafaka kwa wakristo kuwasaidia watu wasiojiweza katika jamii. 

"Tunapoelekea kwenye siku kuu ya pasaka Ijumaa tarehe mosi, ningependa kuwahimiza wakristo kujitokeza kuwasaidia watu wasiojiweza katika jamii," alisema Obare. 

Obare aidha alishtumu hali ya kuongezeka kwa visa vya ufisadi nchini huku akiitaka tume ya kukabili ufisadi kuwachukulia hatua kali wahusika wa uvujaji wa pesa za umma. 

"Visa vya ufisadi vimekuwa vikikithiri katika idara mbalimbali za serikali, na ni ombi langu kwa tume ya kukabili ufisadi nchini kuhakikisha kwamba wanaohusika wanakabiliwa kisheria," aliongezea Obare.